Ni stori iliyoanza kuchukua headlines April 21, 2016 Ikiwa bado tunasubiria taarifa kamili kutoka Mahakamani, sasa Ayo TV ilimpata staa Nay wa Mitego kuthitibisha taarifa hizo za mzazi mwenza, Siwema kufungwa miaka miwili Jela.
Akizungumza staa huyo na ripota wa Ayo TV alisema…>>>’Taarifa nimezipokea ni kweli Mzazi mwenzangu amefungwa na kumbuka nilipoamka tu nikakutana na missed za ndugu zake kadhaa ambao wananifahamu nikahisi kuna kitu maana sio kawaida watu kunipigia mara kwa mara, kumpigia akaniambia Siwema amehukumiwa miaka miwiili Jela sikuamini ikanibidi nimpigie tena ndugu wa karibu naye akanithitibishia hivyo‘ – Nay wa Mitego
‘Kosa unajua mimi nilishasahau kwamba kitu chochote kichotokea kipindi cha nyuma kwasababu ni muda kidogo na pia sikuwa naye kwenye mawasiliano ila niliambiwa kuwa amehukumiwa miaka miwili kutoka na kosa lake, nimejikuta nimekuwa mnyonge nimeingia imani kusikia habari hiyo’ – Nay wa Mitego
Unaweza ukabonyeza play kutazama interview ya Nay wa Mitego akizungumza kuhusu kufungwa kwa Mzazi mwenza miaka miwili Jela