HUYU NDO MTANZANIA MREFU KULIKO WOTE ........ ANAMZIDI HASHIMU THABITI - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Monday, 22 July 2013

HUYU NDO MTANZANIA MREFU KULIKO WOTE ........ ANAMZIDI HASHIMU THABITI


UKIMUANGALIA kwa mara ya kwanza mchezaji wa Tanzania anayecheza timu ya kikapu ya Oklahoma City Sounders inayoshiriki Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), Hasheem Thabit unaweza kujiridhisha kwamba ni mrefu kuliko Watanzania wote uliowahi kuwaona. Ana futi 7.3. Lakini mjini Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani kwenye shule ya Lord Barden yupo mchezaji anayemzidi Hasheem kwa urefu akiwa na futi 7.5. Si mwingine namzungumzia Julius Charles (18) ni maarufu zaidi maeneo ya Bagamoyo, na umaarufu huo umetokana na kimo chake huku wengi wakimuita mpinzani wa Hasheem Thabit kutokana na urefu alionao ambao umepitiliza na ukikutana naye lazima utishike au ubaki ukimshangaa.