Uzinduzi Rasmi wa Mpango wa Kitaifa wa mafunzo ya Uanangenzi(Apprenticeship) katika Hotel ya Hyatt Kempinski ambao una lengo la kuwajengea ujuzi wanavyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu kutokana na fani mbalimbali walizonazo.
Mpango huu unaosimamiwa na Wizara ya Kazi,Vijana na Ajira pamoja na Wadau wengine kama Chama cha Waajiri Tanzania(ATE) na Shirika la GAN la Uswis umelenga katika kumuongezea ujuzi kijana wa kitanzania kwa kupata mafunzo ya vitendo kutokana na fani yake anayoisomea na hivyo kusaidia kutatua kikwazo kikubwa cha "UZOEFU"kinachowakumba wahitimu wa Elimu ya juu pindi wanapotafuta Ajira.
Mpango huu ambao utakuwa chini ya Muongozo wa Kitaifa wa Mafunzo ya Uanangenzi una lengo la kutengeneza utaratibu mzuri kwa vijana kujifunza kwa vitendo kupitia katika Taasisi mbalimbali za binafsi na serikali bila kupata usumbufu wa maeneo ya kazi ya kujifunza kwa vitendo.
Utaratibu huu utapunguza kwa kiasi kikubwa sana usumbufu kwa vijana wa kitanzania kuhangaika kupata maeneo ya kujifunzia kwa vitendo,ambapo kupitia mpango huu wanavyuo watawekewa utaratibu mzuri wa kupata maeneo ya kujifunzia kwa vitendo pasipo urasimu wowote.