Serikali
kupitia Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi katika kipindi cha mwaka 2010-2015
imekamata vyombo 2795,injini za
Mitumbwi 118,magari 297 na pikipiki 33 kwa sababu ya uvuvi haramu na
utoroshwaji haramu kupitia maziwa
makubwa,mwambao wa Bahari ya Hindi na Mipaka ya Nchi.
Hayo yamesemwa
leo Bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha
wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Fakharia Khamis.
“Katika
kukabiliana na wavuvi haramu,Wizara imeanzisha na kuimarisha vituo 25 vya Doria
kwenye Maziwa makuu,Mwambao wa Bahari ya Hindi na mipaka ya nchi”Alisema
Mhe.Ole Nasha.
Aidha amesema
kuwa kuwepo kwa vituo hivyo kumeongeza uwezo wa kukabiliana na uvuvi na
biashara haramu kupitia operesheni mbalimbali
ambapo pamoja na jitihada za Serikali tatizo hili bado linaitaji mkazo
mkubwa sana katika maneo ya mialo na masoko.
Aidha Serikali
imeanzisha kikosi kazi cha Kitaifa Mult
Agency Task Team (MATT) ambacho kinafanya kazi ya kudhibiti uhalifu wa
mazingira ikiwemo kudhibiti uvuvi haramu hususan matumizi ya mabomu katika
shughuli za uvuvi uku pia Maboresho ya Sera,Sheria,na Kanuni za Uvuvi
zikifanyiwa kazi ili kuimarisha usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali za
uvuvi nchini.
Kwa upande
mwingine katika kipindi hicho cha 2010-2015 watuhumiwa 3792 walikamatwa na kesi
243 zilifunguliwa mahakamani ambapo pia jumla ya shilingi 158,559,323 zilikusanywa ikiwa ni
faini kutokana na makosa mbalimbali uku watuhumiwa 11 wakifungwa.
Mhe.Ole Nasha
pia alitoa wito kwa wabunge ambao ni wajumbe katika halmashauri waendelee kutoa
elimu kwa wavuvi kuhusu madhara ya uvuvi haramu, na kuhimiza Halmshauri zao
katika kudhibiti uvuvi haramu kwenye maeneo yao.
“Naziomba
Jamii za Wavuvi na wadau wote washirikishwe katika kusimamia rasilimali za
uvuvi na matumizi endelevu kwa ajili ya kuwapatia wananchi ajira,chakula na
uchumi wao na Taifa kwa ujumla ili kudhibiti uvuvi haramu”Alisisitiza Mhe.Ole
Nasha.