
Kacks Mc ni msanii kutoka Morogoro ambaye anachipukia kwa kasi katika mziki nchini Tanzania ambapo tayari amewahi kutamba na single yake iliyoitwa Mwedokasi iliyotoka novemba 2015.
Sasa mwaka huu 2017 ameamua kutuzawadia single mpya inayoitwa #Moyo aliyofanya kwa mtayarishaji Vent Skillz kisha kuumpa shavu Mash J kuimba kiitikio na vionjo katika wimbo huo.
"nimeandika kuhusu upekee wa kila mmoja kuhusu moyo wake, binadamu tunatofautiana sana ndani ya nafsi zetu nafsi ni siri na hapo moja kwa moja tunanena moyo, kwahyo ni utofauti wa mtu mmoja na mwingine katika chaguzi za mioyo yetu" alisema Kacks kuhusu single hiyo.
Baas the capitaltz.com tumekusogezea mkwaju huo kuusikiliza na kuupakua hapa chini.