
Mr. Masumbuko ndiyo jina la single mpya kutoka kwa msanii Mash Jay, moja ya wasanii wa Hip Hop kutoka mkoani Morogoro.
Akizungumza na Capitaltz.com Mash alisema kuwa kile alichokiimba zaidi ni kuhusu mihangaiko ya hapa na pale ambayo kwa kiasi kikubwa hukwamisha harakati binafsi za Maendeleo.
"Ni Idea ambayo ukiifikiri sana imebeba uhalisia kwa mtu ambaye anahustle bila kujua ni vp atajikwamua pale alipo, ndyo maana ukalikuta jina na Masumbuko hapo"Alisema Mash.
Hata hivyo single hiyo imetayarishwa na Vent Skillz chini ya studio za Kwanza Records.
Hii hapa chini, isikilize na unaweza kuipakua pia...