Serikali imetakiwa kuweka jitihada za ziada ili kupunguza changamoto mbali mbali zikiwemo changamoto za miundombinu ya umeme zinazo jitokeza kwa wawekezaji hususani katika
viwanda vya uzalishaji wa bidhaa mbali mbali nchini.
Changamoto ya umeme imetajwa kuwa ndio kikwazo kikubwa ambayo pengine isipopewa utatuzi mapema inaweza kukwamisha shughuri zote za uzalishaji katika kiwanda hicho hali iliyomfanya mkuu wa wilaya ya njombe Ruth Msafiri kuuagiza uongozi wa halmashauri ya mji makambako kuangalia utaratibu wa kufanya mawasiliano na shirika la umeme ili kuweza kunusuru kiwanda hicho.
Akibainisha baadhi ya changamoto hizo mhasibu Aisha Ismail Kitundu wa kiwanda cha Rosper Company Limited kinachozalisha bidhaa za ujenzi ikiwemo misumari na senyenge kilichopo halmashauri ya mji wa makambako mara baada yakutembelewa na mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri na kuamua keleza baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo.
MICHAEL SHIRIMA ni msimamizi wa kiwanda hicho ambae amesema kuwa licha ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho kupokelewa vyema na mikoa ya nyanda za juu kusini,
kiwanda hicho kinategemea kupanua zaidi wigo wa uzalisha huku akieleza kuwa changamoto ya umeme ndio kikwazo kikubwa katika kampuni.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri ametumia fursa hiyo kuutaka uongozi wa kiwanda hicho kupanua wigo wa uzalishaji zaidi hadi kufikia kiwango cha juu kwa kuwa wananchi kwa sasa wanathamini bidhaa zao za ndani huku akishauri uongozi wa halmashauri kuona namna ya kuwasiliana na shirika la umeme Tanzania Tanesco ili waweze kutatua changamoto ya umeme katika kiwanda hicho.
Katika hatua nyingine msafiri ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kujiongeza zaidi katika maswala ya nishati ikiwa ni pamoja na kutumia njia mbadala ikiwemo ya matumizi ya jenereta
Hata hivyo mwenge wa uhuru unaotarajiwa kuwasili mkoani njombe siku ya tarehe 28
mwezi april na kufungua zaidi ya miradi sita