Bodi ya Ligi kuu Tanzania (TPLB) imefungua malalamiko dhidi ya Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga, Salum Mkemi.
Mkemi ameandikiwa barua ya kuitwa katika kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka nchini, TFF siku ya Jumapili.
Bodi ya Ligi Kuu inamlalamikia Mkemi kwa kutoa kuishutumu kuidhalilisha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, 9 Kamati ya Saa 72 ).
Kupitia vyombo vya habari Mkemi anadaiwa kuishutumu kamati kuwa inaendeshwa kwa unazi na iligubikwa na rushwa katika kushughuluikia suala la kadi tatu za njano kwa mchezaji Mohamed FAkhi wa Kagera Sugar.
Bodi ya Ligi imeambatanisha ushahidi wa video wa matamshi ya Mkemi.