MARIO GOTZE ndie aliwapa Ubingwa wa Dunia Germany huko Brazil alipofunga Bao 1 na pekee walipowabwaga Argentina 1-0 lakini sasa yupo nje ya Uwanja akiugua Ugonjwa ambao umeelezwa ni wa kipekee na nadra kumkumba Binadamu.
Wengi wanakumbuka, Gotze, mwenye Miaka 22, akiunganisha Krosi ya André Schürrle katika Dakika za Nyongeza 30 na kumchambua Kipa wa Argentina Sergio Romero akifunga Bao safi na kuipa Germany Taji kubwa Duniani ndani ya Rio De Janeiro Mwaka 2014.
+++++++++++++++++
JE WAJUA:
-Gotze ni Neno la Kijerumani lililobuniwa Karne ya 16 na Martin Luther akitafsiri Bibilia ya Kilatino.
-Lilimaanisha ‘Mungu Feki’.
+++++++++++++++++
Mwishoni mwa Mwezi uliopita, Klabu yake Borussia Dortmund ilitamka kuwa Gotze amegunduliwa na Ugonjwa nadra kumkumba Binadamu unaoathiri Musuli, kumletea uchovu na Mwili kuongezeka Uzito.
Wiki iliyopita, Dortmund ikathibitisha kuwa Nyota huyo hataonekana tena Uwanjani Msimu huu.
Mashaka ya Gotze kwa sasa yameleta wasiwasi mkubwa kwa Mashabiki wa Germany wakihofia huenda Jina ‘Gotze’ ndilo limeleta nuksi kwenye Maisha yake.