Novat Lufunga beki wa simba sc(mwenye jezi nyekundu)akipigwa chenga na Hamis Tambwe wa Yanga
Msemaji wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara amemkingia kifuoa beki wa kati wa klabu hiyo Novat Lufunga kufuatia makosa aliyoyafanya wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka tanzania bara dhidi ya Young Africans mwishoni mwa juma lililopita.
Haji amemtetea beki huyo kwa kusema kosa alilolifanya na kusababisha penati katika dakika ya tano ya mchezo huo ni la kawaida na hata kama ingetokea Simba wanapoteza dhidi ya mahasimu wao asingemlaumu.
Haji Manara
Amesema beki huyo amefanya kazi kubwa msimu huu, na wakati mwingine wanaomlaumu kwa makosa aliyoyafanya ya kumuangusha Obrein Chirwa wa Young Africans wanapaswa kufikiria na wema wake pia.
Zaidi msikilize hapa chini Manara akizungumza zaidi
