STRIKER MTANZANIA AENDELEA KUTESA ULAYA, APIGA LA TATU DK YA 78 - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Tuesday, 3 January 2017

STRIKER MTANZANIA AENDELEA KUTESA ULAYA, APIGA LA TATU DK YA 78

Picha ya Adi Yussuf

Grimsby Town wamelamba dume !! kwa kauli thabiti yaweza kuwa hivyo baada ya wikiendi iliyopita kukamilisha usajili Kwa mkopo striker Mtanzania Addi Yussuf kutoka Mansfield Town Fc na hatimaye usiku wa kuamkia leo kuwa ni mmoja wa wafungaji wa mabao 3 wakati klabu yake hiyo mpya ikishinda bao 3-1 dhidi ya Carlisle United.

Mabao mengine ya Grimsby yalifungwa na Omar Bogle (48) Omar Bogle (74)

baadhi ya comment kumuhusu Adi baada ya kusajiliwa Grimsby Town
Mshambuliaji huyo ambaye amewahi  kuvitumikia klabu tofauti tofauti vya Uingereza  kama Lincoln City, Oxford City, Crawley Town, anatazamiwa kwenda kujungana  na mwalimu wake wa zamani Mickey Moore katika klabu yake mpya ya Grimsby Town
Adi Yussuf ambaye maisha yake ya soka alianzia kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza Leicester City 2011, alipelekwa kwa mkopo katika timu ya Tamworth baada ya kushindwa kulishawishi benchi la ufundi la Leicester City, pia Adi amewahi kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa Stars chini ya mwalimu Charles Mkwasa kilicho kuwa kikijiandaa na mchezo dhidi ya Chad, japo hakufanikiwa kutinga jezi ya Taifa kutokana na mchezo huo kutochezwa
Picha ya Fadhili Omary SizyaAdi Akiwa Crawley Town Fc
Timu ambayo Yussuf alicheza kwa mafanikio zaidi ni Oxford City miaka ya nyuma, katika michezo 39 ya Ligi alifanikiwa kufunga magoli 27 na ndicho kilicho wavutia klabu ya mansfield kuitaji huduma yake