Uteuzi mwingine alioufanya Rais Magufuli leo..... - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Wednesday, 7 December 2016

Uteuzi mwingine alioufanya Rais Magufuli leo.....

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Desemba, 2016 amefanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja na Mkuu wa Mkoa mmoja na pia amefanya mabadiliko mengine katika Wizara na Mikoa kama ifuatavyo;
Rais Magufuli amemteua Prof. Faustine Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, kabla ya uteuzi huo, Prof. Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu, Mawasiliano.
Rais Magufuli pia amemteua Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo anayechukua nafasi ya Dkt. Frolence Turuka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Frolence Turuka alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliyekuwa akishughulikia Kilimo, na sasa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Aidha Rais Magufuli amemteua Dkt. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na atakuwa akishughulikia Mawasiliano, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Faustin Kamuzora ambaye ameteuliwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mbarak Abdulwakil ambaye amestaafu.
Pia Rais Magufuli amemteua Mhandisi Angelina Madete kuwa Naibu Katibu Mkuu Katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Maria Sasabo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano.
Uteuzi mwingine uliofanywa na Rais Magufuli ni wa kumteua Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Christopher Ole Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe akichukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Dkt. Rehema Nchimbi anajaza nafasi iliyoachwa na Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Dkt. Osward J. Mashindano kuwa Msajili wa Hazina akichukua nafasi ya Lawrance Mafuru ambaye imeelezwa kuwa atapangiwa kazi nyingine.