Kupitia segment ya Chini ya Ulinzi,inayoruka kupitia show ya Gwaride kutoka Abood Fm msanii Koba Mc amefunguka kuwa kutafuta kiki ni mojawapo ya mambo anayoyachukia sana katika muziki wa bongo fleva nchini Tanzania.
Star huyo aliyewahi kutamba na kundi la Watu Pori chini ya nguli wa muziki wa Hip Hop Afande Sele na Dogo Ditto, alijibu swali hilo alipoulizwa kuhusu ni vitu gani huwa vinamkera kwenye muziki wa bongo kwa sasa "kwamba wasanii kiki imekuwa kama ndiyo mtaji sasa, ili upate trend kuongelewa sana watu sasa wanagombania kutengeneza kiki hatimaye wanatengeneza uongo, sababu kitu cha kutengeneza automatically kinakuwa cha uongo vile vile" alizungumza msanii huyo.
Pia Koba Mc amezungumza vitu vingi ikiwemo sababu za wasanii kutengeneza audio mbovu na video kali pamoja akiweka ukweli hata wasanii ambao wamekuwa wakikurupuka kuandika miziki yao.
Zaidi msikilize hapo chini akizungumza katika Interview pamoja na watangazaji Abe Kidunda "Simple Bway" na Jiwe Liganga "Jiwe The Don".