Kampuni ya Multichoice Tanzania wasambazaji wa visambuzi vya kisasa vya DSTV kwa kushirikiana na Kituo cha Radio cha E fm (93.4 E FM) mapema leo wameweza kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi zaidi yay 20 wakazi wa Dar es Salaam walioshinda kupitia maswali maalum yaliyokuwa yakiulizwa na kituo hicho cha radi EFM.
Katika tukio hilo la utoaji zawadi, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Bi. Sophia Mjema aliweza kukipongeza kituo cha EFM na DSTV kwa kufanikisha tukio hilo kwani wameweza kurudisha kitu kidogo kwa jamii na zawadi hiyo ya Kapu la sikukuu litakuwa msaada mkubwa kwa falimia.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka EFM kuendelea mikakati yake kwani tokea kuanzishwa kwake hapa nchini imekuwa radio ya mfano mkubwa na wa kuigwa kutokana na vipindi vyake vya kuelimisha,kufurahisha na kujenga jamii huku akitoa wito pia na kwa wananchi kuendelea kufuatilia kwa karibu vipindi mbalimbali vinavyotangazwa na kituo hicho.
“Nawapongeza EFM na DSTV kwa kuwakutanisha leo hii wananchi wa Dar e Salaam kutoka maeneo tofauti ambao ni wasikilizaji wenu na kufanikiwa kushinda zawadi hizi nono. Kapu hili limenona na litakuwa msaada mkubwa ndani ya nyumba.Pia visambuzi mulivyopata vitawawezesha kuona chaneli mbalimbali ikiwemo televisheni mpya ya kituo cha EFM yaani Etv.” Alieleza Mkuu wa Wilaya huyo.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph wakati wa tukio hilo amebainisha kuwa kupitia kisambuzi chake cha DSTV imemwaga zawadi ya visambuzi vya kisasa vipatavyo 24 pamoja na vifurushi vya mwezi mzima kwa washindi wa shindano hilo la Kapu la Sikuu.
“Washindi hao wataweza kusherehekea Sikukuu ya krismas na mwaka mpya kwa kuangalia chaneli zaidi ya 70 za DStv ikiwemo mpira wa ligi ya Hispania (Laliga) na ligi ya Uingereza” alisema Joseph
Alpha aliongeza kuwa, Multichoice Tanzania haijawatunuku washindi hao 24 wa kapu la Sikuu pekee bali watanzania wote kwa ujumla kwani hivi karibuni walishusha bei za vifurushi vyao kwa wastani wa asilimia 16, huku kifurushi maarufu cha DStv Bomba chenye chaneli zaidi ya 70 kikipunguzwa bei hadi sh.19,975 tu.
Baadhi ya zawadi ‘Kapu la Sikukuu’ vikiwa tayari tayari.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati), akimkabidhi zawadi, Asha Soud ambaye ni mshindi la shindano la Kapu la Sikukuu Dar es Salaam leo, lililoendeshwa na Kampuni ya Multichoice Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Redio cha EFM. Kutoka kulia ni msanii Haji Salum ‘Mboto’ Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph na Mkurugenzi wa EFM, Francis Cizza..
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati), akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa shindano la Kapu la Sikukuu Dar es Salaam leo, lililoendeshwa na Kampuni ya Multichoice Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Redio cha EFM. Kutoka kulia ni msanii Haji Salum ‘Mboto’ Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph na Mkurugenzi wa EFM, Francis Cizza..
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati), akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi za shindano la Kapu la Sikukuu Dar es Salaam leo, lililoendeshwa na Kampuni ya Multichoice Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Redio cha EFM. Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph na Mkurugenzi wa EFM, Francis Cizza kushoto.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akiagana na Mkurugenzi wa EFM, Francis Cizza
Mabalozi wa DSTV, Mboto Irene Paul
washindi wakiendelea kupata zawadi