AUDIO-MAJIBU YA MASH J, AMTAJA MSANII T SIGWER SAKATA LA KUPIGWA CHINI MOKOMOKO MVT, ADAI YUPO TAYARI KUYAMALIZA - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Friday, 30 December 2016

AUDIO-MAJIBU YA MASH J, AMTAJA MSANII T SIGWER SAKATA LA KUPIGWA CHINI MOKOMOKO MVT, ADAI YUPO TAYARI KUYAMALIZA

Picha ya Mash J Mpera Mpera
Mash J

Kuhusu lile tifu la kusitishwa kufanya kazi wasanii wawili kwenye studio ya kwanza records chini ya label ya Mokomoko Movement  Mash J pamoja na Meddy Botion leo hii limechukua sura mpya baada ya msanii Mash J kujitokeza katika Exclussive Interview kupitia Radio Abood Fm na kudai hana mahusinao yoyote na msichana aliyeitwa Jamila ambaye alitajwa kutoka nae kimapenzi zaidi ya Urafiki.

Mash J amedai kuwa anachofahamu ni kuwa msichana huyo alikuwa akitoka kimapenzi na producer Vent Skillz, Meddy Botion na hata msanii mwingine anaitwa T Sigwer.
Picha ya Tea Sigwer
Tea Sigwer

"kitu sio kweli nnachojua Jamila ni shemeji yangu ni demu wa vent skillz wala hakuwa msanii katika studio ya kwanza records kwahiyo nashangaa kwanini mpaka producer vent kaamua kuja hadi radio kuzungumza ishu hizi" alisema Mash J.

Aidha baada ya kutajwa kwa msanii mwingine T Sigwa kuhusishwa katika ishu hiyo ilibidi atafutwe live kujibu kile kinachozungumzwa ambapo alisema kuwa anamfahamu Jamila kuwa ni moja ya watu wanaopenda kufanya muziki na kudai kuwa sio mwanamuziki huku akiweka wazi ni kweli alikuwa katika mahusiano nae lakini ni kipindi cha muda mrefu sana tangu walipoachana.

Pia baada ya mengi kuzungumzwa kauli ya mwisho kwa wasanii hao ukimtoa msanii Meddy Botion wameridhia kupatana endapo atapatikana msuluhishi.

Zaidi Sikiliza hapa chini Interview hiyo na uweze kuipakua bure kabisa