Baada ya kususua kwa takribani
majuma mawili sasa hatimaye hati ya uhamisho ya kiungo Mrisho
Khalfan Ngassa imetua kwenye klabu ya Mbeya City fc asubuhi ya leo
.
Akizungumza
na tovuti ya klabu hiyo muda mfupi uliopita Mwenyekiti wa
City, Mussa Mapunda amethibitisha kutua kwa ITC hiyo kutoka shirikisho la soka
la Oman ikiwa ni siku chache baada ya klabu ya Fanja kumruhusu Mrisho
Khalfan Ngassa kujiunga na kikosi cha City, ambayo pia inajulikana
kama
timu ya kizazi kipya.
Akiendelea
zaidi, Mapunda alisema kuchelewa kufika kwa ITC hii hakukuwa na msuguano wowote
baina ya vilabu hivi viwili kilichokuwa kinatokea ni tofauti ya wakati na
siku za ufanyaji kazi kwenye ofisi kulingana na taratibu za nchi
hizi mbili.
Katika hatua nyingine
Mapunda amesema kuwa maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara dhidi ya Mbao fc uliopangwa kuchezwa jumamosi kwenye uwanja wa
Sokoine jijini hapa yanaenda vizuri huku imani kubwa kwa uongozi
wa City ikiwa ni kushinda mchezo huo hasa baada ya suluhu katika michezo miwili
iliyopita.