Mdau mkubwa wa mchezo wa riadha nchini Wilhem Gidabudai ametangaza kuingia katika kinyang’anyiro cha kuwani nafasi ya ukatibu mkuu wa shirikisho la mchezo huo RT, ambalo mwishoni mwa mwezi huu litafanya uchaguzi.
Gidabudai amesema ameamua kujitosa kuwania nafasi ya ukatibu mkuu wa RT, baada ya kuona mapungufu mengi ndani ya uongozi wa shirikisho, hivyo anaamini endapo atachaguliwa ataweza kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa vitendo.
Wakati huo huo Gidabudai amesema leo atakutana na viongozi wa baraza la michezo na taifa BMT, kwa lengo la kutaka kuelezwa mustakabali wa uchaguzi mkuu wa RT ambao umeanza kugubikwa na Jinamizi la matumizi ya katiba.