S. nduka |
Sonnatha ameyasema hayo wakata akihojiwa na mtangazaji wa kipindi cha Micharazo Time kutoka 98.4 Dodoma fm radio Benedict Ngelangela nakusema amekuwa akifuatilia game kwa muda mrefu lakini amegundua watu wengi wamekuwa wakijinadi zaidi kuliko kufanya kazi kwa bidii hususani katika upande wakinadada.
pia amesema hajaona mtu ambaye anaweza kushindananae kwenye sekta ya uigizaji licha ya kuwa anavitambua vipaji vingi kutoka mkoani Dodoma ambavyo havijapata nafasi ya kusikika na wanauwezo mkubwa wa kuigiza kuliko watu ambao wamekuwa wakijinadi zaidi kwenye mitandao ya kijamii.
alipo ulizwa kuhusu Jackline Materu ambaye anashikilia tuzo ya muigizaji bora wa kike Sonatha alijibu kuwa hamtambui hali iliyopelekea mtangazaji kuongeza list ya majina ya waigizaji wakike wenye majina makubwa mkoani hapo akiwemo Rachel Njingo lakini pia Sonatha alionesha kutouelewa kabisa uwezo wa mwanadada uyo kwa kuguna nakusema yupo tayari kuwataja watu wengine kabisa lakini kati ya watu ambao anawakubali Dodoma hayupo Jack Materu wa Rachel Njingo.