Picha: Mtoto ahudhuria mahafali ya chuo na kupokea PhD kwa niaba ya mama yake aliyefariki - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Sunday, 27 November 2016

Picha: Mtoto ahudhuria mahafali ya chuo na kupokea PhD kwa niaba ya mama yake aliyefariki

whatsapp-image-2016-11-26-at-1-15-03-pm
Mtoto apokea Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine kwa niaba ya Mama yake aliyefariki dunia kabla ya mahafali.

Novemba 25, 2016 Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo kilikuwa na sherehe ya mahafali ya 32 ya chuo hicho katika Kampasi ya Solomon Mahlangu “Nelson Mandela Freedom Square” Mazimbu mkoani Morogoro, kuanzia saa 4:00 asubuhi.Wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu walihitimu masomo yao na kutunukiwa Shahada ya Awali, Shahada ya Umahiri na Shahada ya Uzamivu.

Katika hali ambayo iliyokuwa ni ya kuhuzunisha lakini pia ya kutia moyo, mtoto mmoja alipokea Shahada ya Uzamivu (PhD) kwa niaba ya mama yake aliyekuwa akisoma katika chuo hicho. Mama yake alifariki dunia kabla ya siku ya mahafali hivyo mtoto huyo akateuliwa kupokea shahada hiyo kwa niaba yake.

Sherehe hiyo ilitanguliwa na sherehe ya utoaji zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri sana katika masomo yao “Prize awarding Ceremony” hapo alhamisi tarehe 24 Novemba, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa baraza la Chuo yaani “Council Chamber” uliopo kampasi kuu, kuanzia saa 2:30 hadi saa 4:30 asubuhi.