Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Uingereza, Leicester City inafukuzia saini ya kiungo mkabaji wa klabu ya KRC Genk, Wilfred Ndidi.
Ndidi, raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 19 anatazamiwa kuwa muarobaini wa udhaifu uliopo kwenye safu ya kiungo baada ya kuondoka kwa kiungo mkabaji tegemezi, N’golo Kante.
Aidha huenda Genk wamestukia kufuatiliwa kwa kiungo huyo na kupitia ukurasa wao wa Instagram wameandika na kupost picha yake kuwa "LIKE if you want this man stay at Genk #Ndidiisgenkie "
Leicester City inaripotiwa kuweka mezani ofa ya pauni milioni 15.5 lakini mabosi wa Genk wanataka pauni milioni 19 kumuachia Ndidi.