Mwanafunzi asimulia alivyobakwa na kupewa mimba na Mwalimu - DODOMA - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Sunday, 27 November 2016

Mwanafunzi asimulia alivyobakwa na kupewa mimba na Mwalimu - DODOMA

November 25 umefanyika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo kwa Dodoma yalifanyika katika viwanja vya Nyerere square huku mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme.
Moja ya tukio lililogusa hisia za wengi ni simulizi ya mwanafunzi Joyce Samwel aliyebakwa na mwalimu wake na kisha kumsababishia ujauzito uliopelekea kukatisha masomo yake..
Nilipofika darasa la saba mwalimu Mtajama aliniita ofisini kwake akaniambia ananipenda nikamkatalia na kumwambia mimi nataka kuendelea na masomo akaniambia kama ni kusoma shule nitasomatu‘- Joyce Samwel
Nikamuuliza je, nikipata mimba itakuwaje akaniambia nisiwe na wasiwasi nikipata ujauzito tutalitatua, siku ya pili aliniita nyumbani kwake na nilivyoenda akanivuta chumbani kwake na kunivua sketi‘ –Joyce Samwel
Baadae alinilaza kwenye kitanda chake na kuniingilia kimwili na baadae nikapata ujauzito, nilivyomtaalifu akasema ataongea na wazazi wangu hivyo nisiwe na wasiwasi‘ –Joyce Samwel
Unaweza kuendelea kumsikiliza kwenye hii video hapa chini…..

MANENO YA DC DODOMA KUHUSU MWANAFUNZI ALIYEBAKWA NA MWALIMU