MKE WA RAIS MAGUFULI ALAZWA MUHIMBILI, MAGUFULI AIBUKIA WODINI - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Thursday, 10 November 2016

MKE WA RAIS MAGUFULI ALAZWA MUHIMBILI, MAGUFULI AIBUKIA WODINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mke wake mama Janeth Magufuli aliyelazwa katika Hospitali ya Muhimbili wodi ya Sewa Haji akipatiwa Matibabu Novemba 10,2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali Waziri wa Zamani Balozi Ramadhani Mapuri ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu Novemba 10, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwafariji baadhi ya wagonjwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea kuona wagonjwa pamoja na mkewe ambaye anapatiwa matibabu hapo Novemba 10, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru na kuwapongeza kwa kazi nzuri baadhi ya madaktari na wauguzi kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea wagonjwa pamoja na mkewe ambaye anapatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia mkono wananchi alipokuwa akitoka wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea wagonjwa pamoja na mkewe ambaye anapatiwa matibabu Novemba 10, 2016-Picha na IKULU