Nikiwa na Mstahiki Meya Mh Jaffary Mwanyemba katika kikao cha pamoja na wafanyabiashara wa Stand ya Jamatini na Stand Kuu ya mabasi ya mkoani kwenda kutoa ufafanuzi juu ya alama "X" zilizowekwa katika maeneo yao pamoja na taarifa ya kuondoka maeneo hayo ifikapo tar 16.12.2016
Nimezungumza na uongozi wa RAHCO wamekubali kutowaondoa wafanyabiashara hao tar 16.12.2016 mpaka kwanza vikao vikae baina ya Uongozi wa Manispaa na RAHCO na pia kupitia kamati chini ya Mkuu wa Mkoa ili ufumbuzi upqtikane kwanza.
Kwasasa wafanyabiashara wanaweza kuendelea na shughuli zao mpaka vikao tajwa hapo vifikie makubaliano na maamuzi#MtumishiWaWatu#