Kocha wa Yanga Hans van der Pluijm
Hans Van der Pluijm atakumbukwa sana kutokana na mambo makubwa aliyo yafanya ndani ya Yanga kwa kipindi cha muda mfupi tu

Hans alifanikiwa kuibadilisha Yanga na kuwa moja ya timu tishio kwa soka safi na ushindi wa magoli mengi kwenye mashindano ya  hapa na nje ya nchini

Licha ya mazuri mengi ila Hans amesha wahi kuiingiza hasara klabu kwa kufanya usajili mbovu na usio na faida ndani ya  kikosi cha Wanajangwani

The CapitalTz.Com inakuletea usajili mbovu  wa wachezaji 5  ndani ya kikosi cha Yanga chini ya Hans Van Pluijm

Joseph Zuttah
Alisajiliwa na Hans akitokea Ghana kwa gharama kubwa ila Mghana huyu alishindwa kuendana na kasi ya klabu na kufikia kuwekwa benchi na wazawa, alidumu kwa miezi mitatu pekee kabla ya kutupiwa virago na nafasi yake kuchukuliwa na Thabani Kamusoko ambaye amekuja kuwa na mchango wa moja kwa moja kikosini

Issoufou Boubacar
Muda mwingi alikuwa jukwaani akiuguza maumivu kuliko kucheza hata alipo pata nafasi hiyo alishindwa kuonesha dhamani yake, alifunga goli moja kwenye Ligi huku hakizidiwa na wazawa kwa mbali licha ya mamilioni aliyo chota klabuni

Benedicto Tinocco
Hakufanikiwa kucheza hata mechi moja chini ya Hans hadi kupelekea kupelekwa Mtibwa Sugar kwa msimu huu, alisajiliwa kwa zaidi ya milioni kumi akitokea timu ya maboresho ambayo ilitokana na programu muhimu ya TFF

Paul Nonga
Ni kama aliitia hasara Yanga kwa muda mfupi aliodumu kikosini, mshambuliaji huyu alipendekezwa na Hans hasa baada ya makali yake aliyokuwa nayo Mwadui ila licha ya kuipata saini yake alishindwa kumtumia na Nonga kushuka kiwango kutokana na nafasi ndogo anayoipata

Husein Javu
Alimchukuwa kutoka Mtibwa kwa malengo ya kukiongezea nguvu kikosi kwenye eneo la ushambuliaji licha ya pesa zote kutumika kwenye uhamisho wake ila Javu ulikuwa ni usajili mbaya kwa Hans kwani hakufanya chochote na kuamua kurudi Mtibwa tena