JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI
LA POLISI TANZANIA
YAH:
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO
VYA HABARI TAREHE 06/03/2014.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
limeendelea kufanya msako katika maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata
wanawake wapatao 15 wanaojihusisha na biashara haramu ya kuuza miili yao kutoka
mikoa mbalimbali nchini. Msako huo ulifanyika tarehe 05/02/2014 majira ya
21:00hrs katika mitaa ya uhindini na Air Port. Waliokamatwa katika msako huo
ni:-
1.
VERONICA D/O JOEL mwenye miaka 23,
Mnyakyusa mkazi wa Sai Mbeya.
2.
ROSE D/O MICHAEL mwenye miaka 30,
Mgogo, Mkazi wa Kikuyu Dodoma.
3.
MARIAM D/O JORDAN mwenye miaka 26,
Mhehe mkazi wa Tukuyu Mbeya.
4.
REHEMA D/O RAMANDANI mwenye miaka
38, Mlugulu makazi wa Airport Morogoro.
5.
JOYCE D/O MARTINE mwenye miaka 22,
Mnyamwezi mkazi wa Chinangali West Dodoma.
6.
FATIA D/O SARATIELI mwenye miaka 20,
Mgogo mkazi wa Makanda Bahi Dodoma.
7.
BOKE D/O CHACHA mwenye miaka 27,
Mkurya mkazi wa Tarime Mara.
8.
SWAUMU D/O BAKARI mwenye miaka 23,
Mnyamwezi mkazi Chinangali Dodoma.
9.
ROSS D/O MASAKI mwenye miaka 28,
Mchaga mkazi wa Sanya juu Moshi.
10.
SCOLASTIA D/O COSTANTINO mwenye
miaka 22, Mnyakyusa mkazi wa Gongolamboto Dar es salaam.
11.
HAPPY D/O JULIUS mwenye miaka 31,
Mnyamwezi mkazi wa Urambo Tabora.
12.
AISHA D/O HASSAN mwenye miaka 38,
Mbulu mkazi wa Babati Manyara.
13.
JULIANA D/O DOMINICK Mwenye miaka
31, Mnyakyusa, mkazi wa Airport Dodoma.
14.
DATIVA D/O LUKWEMBE mwenye miaka 29,
Mhaya mkazi wa Kiziba Bukoba Kagera.
15.
DORIN D/O MASSAWE mwenye miaka 23,
Mchaga mkazi wa Kiboshomaro Moshi.
Aidha katika msako huo watu wawili
wanaume walikamatwa wakiwa na mirungi robo kilo katika mtaa wa barabara ya nane
(8) Manispaa ya Dodoma ambao ni NASSOR S/O ALLY mwenye miaka 45, Mwarabu mkazi
wa barabara ya kumi na AYUBU S/O TEPO mwenye miaka 40, Muarusha, Fundi cherehani
mkazi wa Chamwino.
Pia katika Wilaya ya Kongwa kijiji
cha Mlanje kata ya Matongoro Tarafa ya Zoisa alikamatwa mtu mmoja aliyefahamika
kwa jina la SHEDRACK S/O MACHILE mwenye miaka 46, Mgogo, Mkulima akiwa na Lita
30 za pombe ya moshi akiziuza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema msako
unaendelea na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.
