HII NDIO SAFARI YA SALM KIKEKE ILIOMFIKISHA BBC SWAHILI KUWA MTANGAZAJI MWENYE UWEZO MKUBWA NA KUPENDWA, ALISHAWAHI KUCHIMBA MADINI MERERANI BAADAE KUFANYA KAZI BILA MALIPO ...MSIKILIZE HAPA - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Sunday, 16 February 2014

HII NDIO SAFARI YA SALM KIKEKE ILIOMFIKISHA BBC SWAHILI KUWA MTANGAZAJI MWENYE UWEZO MKUBWA NA KUPENDWA, ALISHAWAHI KUCHIMBA MADINI MERERANI BAADAE KUFANYA KAZI BILA MALIPO ...MSIKILIZE HAPA

 Nikiwa ni mmoja ya watu ambao nawapenda na ndoto yangu ni kukutana nae hata kwa kunipa fursa ya kupiga picha pamoja, mara kadhaa nimekuwa nikimuandikia ujumbe kupitia facebook fans page yeke lakini kutokana kuwa na marafiki wengi kama mimi wanaomfuatilia nimeshindwa kupokea majibu ya jumbe zangu nilizokuwa nikimtumia.

Pia nimejikuta nikiiga sauti yake mara kadhaa na kujirekodi hii ni kutokana na kupenda aina ya utangazaji wake, baada ya kumaliza shule Jamhuri high school Dodoma nilitamani sana kusomea fani hii ambayo ndugu yangu huyu leo amekuwa kinara na mchapakazi mzuri kwenye tasnia ya habari. kwa bahati mbaya nilishindwa na kujikuta nikisomea Tekinohama (IT/ICT) ila ndoto yangu bado inajengwa na kuimarishwa na watu kama Salim Kikeke kwani ameeleza alikotoka mpaka kufanya kitu anachokipenda leo ni Mwandishi na Mtangazaji wa Kipindi bora cha Dakika 30, DIRA YA DUNIA TV (BBC swahili)

Na Msofe James (Blogger - www.thecapitaltz.com)

Tafadhali FUATILIA Mahojiano yake aliofanya na kipindi cha The Avenue - TBC ONE TV