DOWNLOAD HAPA FREE
Positive Music for the people ni mradi (Project) ulio chini Stopa The
Rhymecca a.k.a Yokoi mradi huo ukiwa na lengo la kuelimisha jamii
kupitia muziki katika mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakigusa jamii
kwa njia mbalimbali kijamii, kisiasa na kiuchumi. Zimeshuhudiwa nyimbo
nyingi za kuparty, kusema unamiliki gun au benz lakini sio kweli,
unampenda binti ambae uwezo wako
hamuendani, kujisifu mimi mkali kuliko flani na mabo mengine je mwisho wa siku unaifundisha nini jamii yako iliyo maskini yenye kuhitaji elimu ili kukabili maisha maisha magumu yanayowakabili kila siku? Takwimu inaonyesha wengi wanaopenda muziki wa bongo falava ni maskini kitu kinachopelekea hata muziki wetu kutofanya vizuri sana kutokana na mashabiki kutonunua bidhaa za wasanii kikamilifu kutokana na umasikini wao. Mradi wa Positive Music for the People itakuwa inajumuisha nyimbo zenye kuelimisha jamii katika nyanja mbalimbali kutunza mazingira, ajali za barabarani, kujikinga na ukimwi, wanafunzi kuzingatia masomo kwani hakuna njia nyingine ya kuwasaidia zaidi ya kupata elimu, madhara ya pombe, rushwa na mambo mengine muhimu ili mradi kuelimsiha jamii. Katika mradi huu ilishatoka ngoma ya ajali za barabarani inayoitwa “Ajali” ikafuatiwa na “Punguza Mwendo” amabazo zilikuwa zimedhaminiwa na Road Safety Council of Tanzania kusaidia kufanya video na mambo mengine. Kwa sasa kutoka mradi wa Positive Music for the People imetoka ngoma inayohimiza kupiga vita uharamia wimbo unaitwa “Save the elephants and rhinos” iliyotengenezwa na Ben Mwamba kwenye studio za Mpo Africa Dar es salaam. Akizungumza Stopa Yokoi amesema album ya Positive Music for the People inataarajiwa kukamilika katika mwa mwaka huu wa 2014.
Source: DJ CHOKA MUSIC
