Dar
es Salaam. Idara ya Uhamiaji imesema kwa sasa inapata katika kipindi
kigumu katika kutoa hati za kusafiria na kwamba imeamua kuwanyima kabisa
baadhi ya watu na hasa vijana wanaotaka kwenda nje ya nchi. Imesema hatua hiyo inatokana na vijana wengi
kujihusisha na shughuli zisizokuwa halali, zikiwamo biashara ya dawa za
kulevya wanapofika katika nchi za kigeni. Hayo yalisemwa jana na Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara
hiyo, Tatu Burhani, ambaye alisema matukio ya watu kukamatwa na
kutumikia vifungo kwa sababu ya kujihuisisha na shughuli hizo,
yameifanya idara kuwa makini zaidi katika utoaji wa hati za kusafiria.
“Kwa sasa tutakuwa makini sana katika utoaji wa
pasipoti hasa kwa vijana kwa kuwa tumegundua kuwa vijana wengi wakienda
nje ya nchi hawana shughuli za kufanya na badala yake, wanaanza kufanya
kazi zilizo kinyume na sheria za nchi husika,”alisema Burhani.Alisema idara kwa sasa imeanza kuwawekea masharti
vijana ikiwa ni pamoja na ..... SOMA ZAIDI
