![]() |
| Godfrey Mosha pichani. Picha na Maktaba |
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya
Principal Ltd, Godfrey Mosha amesimulia jinsi Benki ya Akiba Commercial
(DCB), tawi la Kariakoo, ilivyoidhinisha malipo ya fedha kwa mtu
mwingine kutoka akaunti yake ndani bila yeye kujua.
Mosha ni mmoja wa washtakiwa katika kesi ya wizi
wa fedha kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya
Tanzania (BoT). Pamoja na wenzake, Bahati Mahenge, Manase Makale, Davis
Kamungu na Eda Makale, wanakabiliwa na kesi ya wizi wa Sh1.86 bilioni
za EPA, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuipitia Kampuni ya
Changanyikeni Residential Complex.
Katika kesi hiyo dhidi ya DCB, inayosikilizwa na
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Warialwande Lema, Mosha
anaidai benki hiyo Sh46.8 milioni, zilizolipwa kwa mtu asiyemfahamu kwa
kutumia hundi nne tofauti na tarehe tofautitofauti....SOMA ZAIDI
