MILLARD AYO AFUNGUKA JUU YA AJALI MBAYA ILIYOWAHI KUMTOKEA MAISHANI. - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Thursday, 27 June 2013

MILLARD AYO AFUNGUKA JUU YA AJALI MBAYA ILIYOWAHI KUMTOKEA MAISHANI.

MILLARD AYO: Amina.
Tulikuwa tunasafiri na basi katika safari za kishule, tulikuwa 60 hivi kwenye basi tukapata ajali ‘Ngongoro crater’ bonde la ufa sehemu inaitwa ‘Malanjo Cross’ ni sehemu hatari sana, yaani tuliingia bondeni, yaani sidhani kama leo ningekuwa hai.
MO BLOG: Hebu Millard tufafanulie zaidi tukio hilo la ajali lilikuaje..?
MILLARD AYO:  Yaani sina la kusema ila kama Mungu asingependa mimi nisingekuwepo duniani, lakini kwa sababu alipenda, ndio maana nipo, hata hili kovu katika kichwa upande wa kushoto lipo. Hapa iliingia chuma, unajua mabasi ya zamani yalikuwa na chuma, sasa ile chuma ilikatika wakati basi likijipiga kwenye mawe kama unavyojua kule ni crater.Kwa kweli ninachokumbuka ni kuwa gari lilipotulia watu walikuwa wakilia na damu zinatiririka na mimi nilikuwa nimebanwa katika hiyo chuma na nilipotolewa sikukumbuka tena nini kiliendelea. Ilikuwa mbaya sana kwa sababu lile basi lilikuwa likibiringika kama chupa, hivyo watu wanatupwa  madirishani na kisha gari linawalalia ndio mazingira watu walivyopoteza maisha.
OMG…!!!