Habari tulizozipata hivi punde zinadai kuwa Mkoa wa Kagera umekumbwa tena na tetemeko la ardhi usiku huu.
Mwandishi wa malunde1 blog Lilian Lukakingira aliyeko Bukoba anasema tetemeko limepita tena bukoba dakika chache zilizopita.
Anasema tetemeko hilo siyo kubwa kama la jana na kwamba watu wengi wametoka ndani ya nyumba zao kwa haofu ya kuangukiwa na nyumba.
Mpaka sasa hakujaripotiwa madhara ya tetemeko hilo.
Endelea kutembelea Malunde1 blog kwa habari za ukweli na uhakika