
Muimbaji wa RnB kutoka Marekani, Trey Songz anatarajiwa kuungana na wasanii wengine wa Afrika ambao watashiriki kwenye msimu wa 4 wa kipindi cha Coke Studio Africa.
Uongozi wa kipindi hichi umetangaza habari hii nzuri Instagram “BREAKING NEWS: Joining Coke
Studio Africa Season 4 is singer, songwriter, record producer and actor… @treysongz! Follow the conversation on #CokeStudioAfrica.”
Trey Songz ni msanii wa tatu kutoka Marekani kushiriki kwenye Coke Studio Africa baada ya Wyclef Jean na Ne-Yo.
Trey Songz atafanya collabo na rapa wa Afrika Kusini ‘Emtee‘ na collabo hii itatayarishwa na DJ Maphorisa. Show Ya Trey Songz itakuwa kwenye fainal ambayo ni Episode ya 13 kurushwa 19 November 2016
Tanzania msimu huu inawakilishwa na Vanessa Mdee, Joh Makini, na Yamoto Band huku Diamond akishiriki ile ya Afrika Kusini (Coke Studio South Africa).