MANENO YA NAY WA MITEGO BAADA YA SHAMSA FORD KUOLEWA - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Saturday, 3 September 2016

MANENO YA NAY WA MITEGO BAADA YA SHAMSA FORD KUOLEWA

Share this

Hakuna asiyejua kama mwanadada wa Bongo Movie Shamsa Ford na rapper Nay wa Mitego kwamba walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi hapo awali.
Mwanadada huyo hapo jana ameweza kufanikiwa kutimiza nusu ya dini kwa imani ya dini yake kwa kufunga pingu za maisha (Ndoa) na mfanya biashara maarufu wa nguo jijini Dar es Salaam Chidi Mapenzi.

Shamsa f
Mwanadada Shamsa Ford kwenye harusi yake
Shamsa Fo
Shamsa na mumewe Chidi mapenzi

Kama ilivyo kawaida kwa mtu yeyote hali inakuaga sio nzuri pale mtu ambaye ulikuwa naye katika mahusiano anapoamua kupiga hatua na kufanya maamuzi magumu kwa kufunga ndoa na mtu mwingine bila kujalisha kwamba mwanadada Shamsa Ford na Nay wa Mitego walikwisha utangazia umma kwamba wao hawapo tena kwenye mahusiano na kilichobaki ni urafiki wa kawaida tu.
Na hicho ndicho kiliwasukuma watangazaji wa kipindi cha D’Wikend Chatshow cha Clouds TV Qwhisar naSoudy Brown kumpigia simu Nay wa Mitego na kutaka kumjulia hali yake. Na hiki ndicho alichokisemaNay wa Mitego.
“Namtakia kila la kheri lakini wakiachana atarudi tu. Hatuombi waachane lakini kuna hapa na pale inaweza kutokea endapo wakishindwana me ntampokea kwa mikono miwili.”

Dondosha neno moja tu kwa Nay wa Mitego kwa uamuzi wake huo ambao kauchukua.