MAN 2 MAN!!! KUNUNA AU KUCHEKA, EUROPA LEAGUE RATIBA NZIMA NA DONDOO MUHIMU ZIKPO HAPA - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Wednesday, 14 September 2016

MAN 2 MAN!!! KUNUNA AU KUCHEKA, EUROPA LEAGUE RATIBA NZIMA NA DONDOO MUHIMU ZIKPO HAPA



 Image result for jose mourinho action
KEPTENI wa Manchester United Wayne Rooney hayumo kwenye Kikosi cha Timu hiyo kilichoruka kwenda Rotterdam kucheza na Klabu ya Netherlands Feyenoord katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI.

Wengine ambao hawamo kwenye Kikosi hicho cha Wachezaji 20 ni Luke Shaw, Antonio Valencia na Jesse Lingard.

Maneja Jose Mourinho amesema Rooney amecheza Mechi zote za England na Man United na hivyo amepumzishwa ile awe freshi kwa ajili ya tripu yao ya Ugenini hapo Jumapili wakicheza kwenye EPL, Ligi Kuu England na Watford.

Kuhusu ushiriki wao kwenye Mashindano haya, Morinho amekiri Klabu haikutaka kuwemo lakini maadamu wamo basi watawania kutwaa Ubingwa.

Ameeleza: "Si ndoto ya kila Mchezaji mkubwa lakini hatumo CHAMPIONZ LIGI. Lazima tuyatizame Mashindano haya kwa heshima. Tunataka tufanye vyema!"

Mbali ya Marcus Rashford kuanza Mechi hii kama Mourinho alivyodokeza, wengine wanaotarajiwa kucheza ni Marcos Rojo atakaechukua nafasi ya Luke Shaw pamoja na Michael Carrick, Matteo Darmian, Timothy Fosu-Mensah na Memphis Depay.

=============
JE WAJUA?
Man United imeshacheza na Feyenoord mara 2, kwenye Kundi lao la UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu wa 1997/98, na Man United kushinda Mechi zote mbili ikiwemo 3-1 huko Uwanjani De Kuip ambako Andy Cole alipiga Hetitriki.
==============

Wakati huo huo, Feyenoord wamelazimika kupunguza uwezo wa Uwanja De Kuip na kuwa na Watazamaji 30,000 tu ili kukwepa Adhabu zaidi toka UEFA kwani kwa sasa wapo kwenye Angalizo baada ya fujo za Mashabiki wao Msimu uliopita na kupunguzwa huko kutasaidia udhibiti wa fujo za Mashabiki. 

Manchester United - Kikosi cha Wachezaji 20: De Gea, Romero, Johnstone, Darmian, Bailly, Blind, Fosu-Mensah, Rojo, Smalling, Carrick, Fellaini, Herrera, Mata, Memphis, Pogba, Schneiderlin, Young, Ibrahimovic, Martial, Rashford.

UEFA EUROPA LIGI
Mechi za Ufunguzi
Alhamisi Septemba 15
KUNDI A: Feyenoord v Manchester United, Zorya Luhansk v Fenerbahçe
KUNDI B: Young Boys v Olympiacos, APOEL v Astana
KUNDI C: Mainz v St-Étienne, Anderlecht v Qäbälä
KUNDI D: AZ Alkmaar v Dundalk, Maccabi Tel-Aviv v Zenit
KUNDI E: Viktoria Plzeň v Roma, Astra Giurgiu v Austria Wien
KUNDI F: Rapid Wien v Genk, Sassuolo v Athletic Club
KUNDI G: Standard Liège v Celta Vigo, Panathinaikos v Ajax
KUNDI H: Konyaspor v Shakhtar Donetsk, Braga v Gent
KUNDI I: Salzburg v Krasnodar, Nice v Schalke
KUNDI J: Qarabağ v Slovan Liberec, PAOK v Fiorentina
KUNDI K: Inter Milan v Hapoel Beer-Sheva, Southampton v Sparta Praha
KUNDI L: Osmanlıspor v Steaua Bucureşti, Villarreal v Zürich