Meneja Ofisi kuu ya Utabiri wa Hali ya hewa Tanzania (TMA) Samweli Mbuya akizungumzia mabadiliko ya tabia ya nchi kwenye Clouds 360 alisema kuwa, Ongezeko la joto ambalo tunalishuhudia sasa litaendele hadi mwezi wa sita ambapo ndio joto litaanza kupungua.
Joto huongezeka sana pale ambapo jua linakuwa karibu na uso wa Dunia (Jua la utosi). Hali hii hutokea mwezi wa tatu na mwezi wa tisa. Wakati huu jua linakua kwenye mstari wa Equator na sasa linatoka kusini kwenda kaskazini.
Dar kinachosababisha ongezeko la joto ni uwepo wa bahari ila kwa jana Mkoa uliokua na joto zaidi ni Kilimanjaro (Moshi). Katika utendaji wetu hua tunafanya kazi kwa ukaribu na Wizara ya Kilimo lakini pia na taasisi nyingine zinazojishughulisha na mazingira.
Hali ya hewa ikibadilika inabidi wakulima waelekezwe ni mbegu gani za kupanda zitakazoendana na hali ya wakati huo ndio maana tunafanya kazi kwa ukaribu na Wizara husika. Tunawaomba Watanzania waendelee kufuatilia taarifa zetu kuweza kufahamu zaidi kuhusu tabia ya nchi.