JE UNAPENDA KUWA MTANGAZAJI? SOMA HII… - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Friday 2 June 2017

JE UNAPENDA KUWA MTANGAZAJI? SOMA HII…

ezden2
Naamini kwema kabisa huko utokako, nami pia niko salama kabisa namshukuru Mungu. Sasa nimekaa nimefikiria sana jinsi ambavyo kuna ugumu sana nilipitia wakati naanza kuingia katika fani ya utangazaji, takribani miaka 9 sasa ikiwa ni pamoja na kushiriki mashindano mbalimbali ambayo yote leo hii nikitazama nyuma nauona mchango wake hapa nilipo na kinachoendelea juu ya uwezo na uzoefu katika kazi hii iwe kwenye Radio au TV nilioupata Kiss FM, Votu Radio, Times FM, EFM, Star TV, TV Tumaini na TV1.
Kutoka kufanya show za muziki kwa miaka mitatu yote ya kiss fm mpaka kuanza kufanya Drive Time ya Times fm (Maskani) producing and co-hosting with Gadna G Habash kulinibadilisha sana kwani pale ule utangazaji wa “kisela” ukaanza kutoweka na kuanza kujua kufanya vipindi serious vinavyosikilizwa na “matured people” na hata ikawa rahisi sana kushinda katika auditions za TV1 kufanya a very matured Talk show “The One Show” nikiwa na Jokate Mwegelo mwanzo na baadae TeeJay.
Sasa stori kwa ufupi ni kwamba utangazaji ni katika kazi pendwa sana duniani, kitu ambacho kinafanya vijana wengi wakimbilie kwa kuwa inspired na wale walio tayari katika media kwa muda kadhaa. Ni jambo zuri kuvutiwa na mafanikio ya wengine lakini kwa wengi sana fani hii imeanza kuleta taswira kuwa ni ya kawaida sana hasa siku hizi kwa kuwa na watangazji wengi ambao hawapendi na hawataki kusoma vitabu mbalimbali, wanatangaza hasa muziki na kufanya sasa wagodo zetu wengi majumbani hata wale walioko vyuoni wakisomea fani hii kuona kwamba to be a media personality is to broadcast about music na kutoona kama being on such position you are a full journalist, unaweza kuandika, kutengeneza makala mbalimbali na uwezo wa kuyachambua yaliyo katika jamii na kuyafanya kipindi watu wakasikiliza wakaelemika na burudani pia.
Kitu ambacho ukiangalia kwa undani kinapoteza ile ladha ya fani yenyewe kwani wengi wa wanaokuja sasa hata wanaiga mpaka uongeaji wa baadhi ya watangazji waliopo kwenye media mbalimbali. Sasa hapa najiuliza sana kuhusu watangazaji wetu hapo baadae kama hawa waliopo vyuoni wanamtazamo wa kuwa kama fulani wanayemsikia leo. If you wanna be somebody else, then who’s gonna be you???!!! Think and take action.
Ukiniuliza nikupe mfano wa ninachotamani kukiona….. japo wengi wanafanya vizuri lakini to experience the true spirit of a media personality mtazame/ mfuatilie Fredrick Bundallah (Sky Walker) halafu uniambie unaona nini… haya tuendelee…
Sasa, katika wimbi hili la copy and paste kazi zitaendelea kuwa ngumu sana na hazitakuwepo kabisa kama umalize chuo na degree yako ya mass com and broadcasting uje kuomba kazi ukiwa una-sound kama fulani tuliyenae halafu huna ubunifu wowote zaidi ya huyo mtu sababu umeamua kuwa kivuli cha huyo mtu ila fahamu kuwa kivuli hakiwezi kunyooka kama mti umepinda.
Kwahiyo baada ya kuyaona haya yote, na kusoma zaidi kuhusu fani hii ambayo imekuwa ndoto kubwa sana maishani mwangu ambayo naiishi kwasasa naona naweza kusaidia baadhi ya wale ambao wanaipenda fani wasipotee at least wawe na mtazamo sahihi na walete ubunifu unaotakiwa kwa kuwaongoza wasome vitu gani wafanye mazoezi gani na wajifunze vitu gani, wawe watu wa aina gani na je watawezaje kuitimiza ndoto yao ya utangazaji hata kama ajira hakuna???? Kuna intenet sasa hivi ukiwa na kipaji na unajua kuitumia its a free platform ya wewe kupata jina na kutengeneza kipato kwa value ambayo unaweza kuwapatia watu na wakaiona.
kwasasa nina studio yangu mwenyewe ambayo ni ndoto ya miaka mingi sana iliyotimia ambapo natengeneza matangazo mengi sana ya biashara lakini kingine ni kutengeneza vipindi vya radio na kusaidia wale wenye ndoto na vipaji kufikia malengo na hata kutengeneza kipato mtandaoni kwa kuwa na kipindi chako (podcast) kwa gharama nafuu sana na kuna habari njema Tanzania kuhusu hizi Podcast nitaongelea zaidi katika mwendelezo wa makala hii na kwenye Podcast nitakayoitoa soon.
Hii ni sehemu ya kwanza ya makala hii, nimeigawa kwa sehemu ya kwanza utangulizi halafu shemu ya pili tupeane dili.
Haya kama umeanza kunielewa nicheki kwa mawasiliano hapo chini. Kuwa juu ya uwezo wako, it’s time to RUN YOUR SHOW.
Share hii kwa wale wapenda utangazaji…. asante na karibu sana. Usikose part 2.

SIMU: (+255)-759-191-076
EMAIL : ezdenjumanne@gmail.com