Yanga
Africans wamefanikiwa kurudi kileleni katika msimamo wa ligi kuu Vodacom Tanzania
bara baada ya kuifunga bao 2-0 timu ya Tanzania Prisons katika mchezo
ulimalizika jioni ya leo uwanja wa taifa Dar Es Salaam
Yanga sasa wametimiza pointi 59 sawa na Simba lakini
wakirejea kileleni kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Yanga waliingia dimbani wakiwa na shauku ya kuzichukua pointi hizo tatu muhimu huku Prisons
wakionekana kucheza kwa tahadhari kila wakakati.
Kipindi cha kwanza kilimalizika bila ya kufungana licha ya Yanga
kutawala zaidi pambano.
Mabadiliko ya kipindi cha pili ya kumtoa beki Hassan Kessy na
kumpa nafasi Juma Abdul na pia kumuingiza Haruna Niyonzima kuliiongezea kasi
safu ya ushambuliaji ya Yanga.
Mshambuliaji Amissi Tambwe alifanikiwa kuunganisha kwa kichwa
krosi ya Juma Abdul kutokea upande wa kushoto mnamo dakika ya 71.
Dakika nne baadaye Obrey Chirwa aliihakikishia Yanga ushindi kwa
bao lake la kumi na la pili alipomalizia kazi nzuri ya Haruna Niyonzima.
Matokeo mengine:
Toto Africans 2-1
Jkt Ruvu
Ruvu Shouting 1-1
Kagera Suger
Majimaji 3-0 Mwadui
Fc
Ligi hiyo
itaendelea kesho kwa mchezo mmoja ambapo Simba sc itacheza na African Lyon
katika uwanja wa taifa Dar es salaam.