
Dada pumzisha mwili wako ndiyo single mpya ya Nikki Mbishi ambayo kwa siku za hivi karibuni imekaa nafasi ya kwanza katika chati za muziki kupitia mtandao wa Mdundo.Com.
Leo hii msanii huyo kupitia account yake ya twiter alikuwa akirusha madongo kwa wasanii wenzake ambao baadhi yao wanafanya vizuri katika game na wengine wamepotea kwa sasa wakiwa hawana single walizotoa, msanii huyo akawashtua mashabiki wake kwa kuandika kuwa "Nataka nitoe ngoma yangu ina chorus mwanzo mwisho hamna verse maana tumeambiwa tusiimbe maneno mengi mafanzi hawapendi" aliandika hivyo.
Aidha katika baadhi ya madongo ya tweets aliyoandika msanii huyo "Oi dj d'ommy bonyeza #majiyashingo ya daz nundazi iwe maalumu kwa mwanangu @king_zillah " "Bongo Bahati Mbaya verse mistari miwili chorus x 800 #Komesho sio Commercial tena. #Nawaza Tu" "Stamina wa watu maskini kuimba hawezi ila hana namna itabidi tu aimbe la sivyo atarudi Uluguruni kama Izzo Mbeya"
Hata hivyo Nikki Mbishi alihitimisha kwa tweet kuwa "Leo nadiss tu ukimind K*nya chuma, maana kimuziki huniwezi".