KOCHA Mkuu wa Prisons ya Mbeya, Abdallah Mohammed ‘Bares’
amesema kwamba wataing’oa Yanga katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
kocha huyo amesema kuwa anawaheshimu Yanga SC kama timu kubwa
na mabingwa wa Tanzania, hivyo wanajua mchezo utakuwa mgumu, lakini
watajitahidi kupigania ushindi.
Yanga watakuwa wenyeji wa Prisons Jumamosi Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho wa Robo Fainali ya Kombe la ASFC kutafuta
tiketi ya kuungana na Simba, Azam FC na Mbao FC ambazo tayari zimetinga Nusu
Fainali ya michuano hiyo.