VIJANA WA MORO WATUA KWA KISHINDO, NI BAADA YA KUCHUKUA UBINGWA WA AIRTEL RISING STARS, PICHA ZIPO HAPA - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Monday, 12 September 2016

VIJANA WA MORO WATUA KWA KISHINDO, NI BAADA YA KUCHUKUA UBINGWA WA AIRTEL RISING STARS, PICHA ZIPO HAPA



Wakazi wa manispaa ya morogoro leo hii wamejitokeza kuilaki timu ya Mkoa wa Morogoro iliyofanikiwa kubeba taji la michuano ya Airtel Rising Stars siku ya jana ilipoichapa timu ya mkoa wa Ilala bao 1-0.

Akizungumza wakati akikabidhiwa kikombe cha ushindi na timu hiyo mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi Regina Chonjo amewapongeza vijana hao kwa ushindi walioupata huku akiwataka wazazi na walezi kutoa fursa kwa watoto kushiriki kwenye michezo.

Naye mstahiki meya wa manispaa ya morogoro ambaye ni mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa morogoro Pascal Kihanga amesema kuwa mkoa wa morogoro umekuwa na historia nzuri katika michezo licha ya kutokuwa katika ushirikiano kwenye siku za hivi karibuni na akatoa shukrani kwa taasisi sita zilizounda wachezaji hao.