
Medy Botion ni mkali wa hip hop kutoka Morogoro ambaye kashinda
shindano la Super Nyota mkoani humo ikiwa ni maalumu kwa shoo za Fiesta
na moja kwa moja anakwenda jijini Dar es Salaam anakokutana na wakali
wengine kutoka mikoa tofauti tofauti nchini Tanzania.
The CapitalTz.com tumekusogezea
kipande cha interview aliyowahi kufanya katika kituo cha Abood Fm
Morogoro, kwenye shoo ya Mega Mix ambayo inaongozwa na Abedy Maulidy
Kidunda "Simple Bway", Isaya Mdangu "Star Fake" na dj Ndevu akiwaonyesha
umahiri wa mistari ya papo kwa papo "Freestyle" pamoja na uwezo wake wa kuandika mashairi.
Mpaka sasa Medy Botion anatamba na single yake mpya 16 Barz ambayo tayari ametoa na video ya wimbo huo.