REMY KWELI MAJANGA, KATIKA MKOPO WA MSIMU MZIMA ACHUKUA SIKU 9 KUREJEA KLABU YAKE ILIYOMPELEKA - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Friday, 9 September 2016

REMY KWELI MAJANGA, KATIKA MKOPO WA MSIMU MZIMA ACHUKUA SIKU 9 KUREJEA KLABU YAKE ILIYOMPELEKA

Image result for loic remy action injury
Loic Remy amerejeshwa Klabuni kwake Chelsea Siku 9 tu baada ya kuwa kwa Mkopo huko Crystal Palace bila kucheza hata Mechi moja baada ya kuumia.

Reny, Raia wa Ufaransa mwenye Miaka 29, aliumia Pajani Mazoezini Majuzi Jumatatu na sasa amerejeshwa Klabuni kwake Chelsea kupata matibabu zaidi.

Palace imethibitisha tukio hili na kusema atakuwa nje kwa Wiki kadhaa.

Meneja wa Palace, Alan Pardew, amesema: “Kwa bahati mbaya Remy aliumia Mazoezini Jumatatu. Si vibaya sana lakini Wikiendi hii hawezi kucheza na sijui atakuwa nje kwa muda gani hadi vipimo vikamilike.”

Remy alijiunga na Chelsea Mwaka 2014 na kufunga Bao 8 katika Mechi 32.