MALIPO NI DUNIANI, DAVID LUIZ AMSHUKURU SHABIKI WAKE ALIYEKUTANA NAE MIAKA MITANO ILIYOPITA - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Wednesday, 21 September 2016

MALIPO NI DUNIANI, DAVID LUIZ AMSHUKURU SHABIKI WAKE ALIYEKUTANA NAE MIAKA MITANO ILIYOPITA


David Liz amemshukuru kijana ambaye aliwahi kusalimiana nae miaka mitano baada ya yeye kutoka uwanjani akielekea hotelini.

Luiz anasimulia kuwa siku hiyo kijana huyo alimpongeza kwa mchezo mzuri kisha akamuaga usiku mwema, anaendelea kueleza mpaka sasa miaka mitano imepita na wiki iliyopita kwenye mchezo dhidi ya Liverpool alishangaa akiwa anafika hotelini kumwona mtu akikimbia huku akimwita jina lake huku akimwambia “subiri” “subiri” na alipomtazama kwa karibu akamkumbuka kijana mdogo na kujua sahivi amekuwa mkubwa na akamueleza maneno yale ya mara ya kwanza alipokutana nae.

Zaidi ya yote ni jana usiku kwenye mchezo dhidi ya Leicester city Luiz anasimulia kuwa alimshuhudia kwa umakini kijana huyo na kugundua kweli amekuwa mkubwa na zawadi pekee aliyoamua kumzawadia ni jezi yake .

                              Tazama mahiri wa Messi akimpiga tobo Luis Suarez Mazoezini