Hii hapa Kauli ya Serikali kuhusu Askari wanaofanya Mazoezi Barabarani - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Thursday, 15 September 2016

Hii hapa Kauli ya Serikali kuhusu Askari wanaofanya Mazoezi Barabarani

Kutoka bungeni Dodoma September 14 2016 Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba alisimama kutolea kujibu swali la mbunge wa viti maaalum CHADEMA Maryam Msabaha aliyetaka ujua sababu za baadhi ya askari polisi kuonekana wakifanya mazoezi katika maeneo ya wazi ikiwemo barabarani.
Kwanza vikosi vya ulinzi na usalama kufanya mazoezi ni sehemu ya maisha yao, hili la kusema kufanya barabarani ni kuonyesha udhaifu wao ukweli ni kwamba hiyo ni sehemu ya kukabiliana na waharifu‘ -Waziri Nchemba
Mwananchi yeyote ambaye havunji sheria hana haja ya kushtuka kwakuwa askari wanafanya hivyo kwa ajili ya waharifu na mtu asiyekuwa mwarifu hana sababu ya kuogopa‘ Waziri Nchemba