FAHAMU KUHUSU RAPA WAKAZI KUFANYA KAZI KWA MGOMBEA URAIS MAREKANI, AMTAJA HASHEEM THABEET KUMSAIDIA MAHITAJI YAKE - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Friday, 16 September 2016

FAHAMU KUHUSU RAPA WAKAZI KUFANYA KAZI KWA MGOMBEA URAIS MAREKANI, AMTAJA HASHEEM THABEET KUMSAIDIA MAHITAJI YAKE



 Image result for WAKAZI
Rapa kutoka Bong, Wakazi, amesema wakati yuko masomoni nchini Marekani alishawahi kufanya kazi kwenye Hoteli ya Mgombea Urais wa sasa wa nchi hiyo kupitia chama cha Republican, Donald Trump.

Akiongea kupitia kipindi cha Campus Vibes cha Times Fm Jana usiku, Wakazi amedai kuwa Hoteli hiyo iliyopo mjini Chicago ndio ilimpa nafasi ya kukutana na Mastaa wengi zaidi wakiwemo Kanye West, Floyd Maywether, Diddy na Wengine Kibao.

“Nilikuwa tu Door man (Mfungua milango) shughuli zangu ni Front Desk, kwa hiyo nikapata kazi Trump Tower ya Donald Trump, yeye mwenyewe aliwahi kuja siku ile tu inafunguliwa ila watoto wake nimeshakutana nao sana” Alisema Wakazi.

Wakazi aliendelea kusimulia kuwa tabia kubwa ya Bilionea Trump, ni kusoma Magazeti kila siku alfajiri saa 11 na dakika 45, hivyo alikuwa akitumwa kumpelekea Magazeti Chumbani kwake kila siku asubuhi lakini kwa masharti ya kutokushikana mikono.

“Nilikuwa nampelekea Magazeti kila siku saa 11 ukifika hamuongei wala kushikana mikono, anafungua milango alafu wewe unayaweka chini, ilikuwa ni tabia yake huwa hapendi Kushake ‘hands’.”

Katika hatua nyingine rapa huyo ameongeza, kuna kipindi aliamua kuacha kazi kwa tajiri huyo ili ajihusishe zaidi na muziki huku Mcheza kikapu Mtanzania Hashim Thabeet akimsaidia baadhi ya Mahitaji.