Mwanamuziki nguli wa Muziki wa Dansi nchini Tanzania "Ndanda Kosovo" amefariki Dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali zinasema marehemu alifikishwa hospitalini hapo kupata matibabu ya Vidonda vya tumbo vilivyokuwa vikimsumbua siku chache zilizopita lakini alifariki mapema asubuhi ya leo.
Akizungumza na Mwandishi wetu, Mmoja wa Viongozi wa Wanamuziki wa Kongo chini Tanzania, King Dodoo amethibitisha kutokea kwa msiba huo na kusema kuwa Ndandaa kosovo alifikishwa Hospitali ya Mwananyamala juzi na kulazwa tatizo la maradhi ya tumbo.
Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya, jana alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako mauti yamemkuta leo asubuhi.
Ndanda Kosovo aliwahi kutamba na Bendi ya Wajelajela Original miaka ya 2000 na atakumbukwa kwa nyimbo kama, Jela, Chini Ya Uunzi, Chozi La Mnyonge na nyingine nyingi.
“NDANDAA KOSOVO APUMZIKE KWA AMANI!”