POLISI ALIYETAPELI VIJANA 12 AKAMATWA - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Saturday, 16 April 2016

POLISI ALIYETAPELI VIJANA 12 AKAMATWA


JESHI la polisi mkoani Mbeya, linamshikilia askari wake wa kituo cha Mbalizi kwa tuhuma za kuhusishwa na tukio la udanganyifu.
Askari huyo, ambaye jina na namba zake za kazi vimehifadhiwa kutokana na sababu za kiuchunguzi, alikamatwa juzi na kuwekwa chini ya ulinzi, baada ya kutajwa na mtuhumiwa Franky Mushi, kuwa ndiye aliyechukua fedha za vijana 12 kwa ahadi ya kuwapatia nafasi ya kujiunga na jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula alisema baada ya kukusanya fedha kwa vijana hao, aliwaandalia safari ya kwenda Chuo cha Mafunzo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
“Baada ya kukamilisha mipango yao, waliwasafirisha vijana hao Aprili 12, mwaka huu kwa kutumia basi la Kampuni ya HOOD na kiongozi wao alikuwa Mushi ambaye ni askari mgambo,” alisema.
Alisema baada ya Franky kukamatwa, alimtaja askari huyo kuwa ndiye aliyewahaidi kupata nafasi ya kujiunga na jeshi hilo, ambapo kila mmoja alitoa Sh 57,500 mbali na nauli waliyoitumia kusafiri kufika Mbeya hadi Kilimanjaro.