HISTORIA YAITESA BARCA CHAMPIONS LEAGUE - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Thursday, 14 April 2016

HISTORIA YAITESA BARCA CHAMPIONS LEAGUE


FC Barcelona ambao walikuwa mabingwa watetezi wa taji la klabu bingwa Ulaya wamevuliwa ubingwa huo na Antoine Griezmann baada ya kuwashanga kwa kichapo cha magoli 2-0 kwenye mchezo wa marudiano wa robo fainali na kuikatia tiketi Atletico Madrid kucheza nusu fainali ya michuano hiyo ya Ulaya.
Barcelona ilitua kwenye jiji la Madrid ikiwa mbele kwa magoli 2-1 kutoka kwenye mchezo wa awali lakini kutokana madhaifu ya safu yake ya ulinzi, wamejikuta wakiruhusu Griezmann kufanya yake kwenye uwanja wa nyumbani.

Barca walinyimwa penati dakika za lala salama baada ya Gabi kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Kichapo hicho kimefuta ndoto za Barca kutwaa mataji matatu (treble) ya La Liga, Champions League na Copa del Rey ndani ya msimu mmoja kama walivyofanya msimu uliopita huku wakiiacha Atletico kuungana na Bayern Munich, Manchester City na Real Madrid kufuzu kwa hatua ya nusu fainali.
Draw ya kujua timu zipi zitapambana katika hatua ya nusu fainali itachezeshwa siku ya Ijumaa.
Hstoria inajirudia

Mchezo huo ulikuwa ni wa nane kuzikutanisha Atletico Madrid na Barceolna ndani ya miezi 15, huku Barcelona ikiwa imeshinda michezo saba iliyopita.
Hata hivyo usindi wa hivi karibuni wa Atletico dhidi ya Barcelona ulikuwa ni kwenye michuano ya Champions League kwenye hatua kama hii miaka miwili iliyopita.
Barcelona walitupwa nje ya michuano ya Ulaya kwa tofauti ya magoli 2-1 kwenye kichapo cha mwaka 2014 msimu ambao kikosi cha Diego Simeone kilifika hatua ya fainali na kupoteza mchezo mbele ya Real Madrid kwa bao 4-1 kwenye dakika 30 za nyongeza.
Simeone natarajia kikosi chake huenda kikaenda hatua nyingine mbele zaidi.
Majanga yaendelea kumwandama Messi
Messi ameendelea kusalia kwenye rekodi yake ya kufunga magoli 499 kwenye maisha yake ya soka ambayo aliiweka tangu March 30 alipoifungia goli timu yake ya Argentina.
Ameshacheza jumla ya dakika 452 bila kufuifungia goli klabu yake ya Barcelona.
Kwenye mchezo wa Jumatano, Messi hakuonekana kutaka kufunga kwasababu alishindwakupiga shuti hata moja lililolenga goli kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Champions League tangu mwaka 2014 ambapo ilikuwa dhidi ya Atletico.
Nyota huyo mwenye miaka 28 alikuwa chini ya uangalizi mkali wa Godin na Lucas Hernandez ambao walikuwa kwenye kiwango bora kwenye safu ya ulinzi ya Atletico.
Takwimu muhimu za mchezo;

  • Hakuma timu yeyote ambayo imewahi kutetea taji la Champions League tangu lilipopewa jina jipya msimu wa 1992/93.
  • Diego Costa pekee ndiye mchezaji wa Atletico Madrid aliyeweza kufunga magoli nane (8) kwenye michuano ya Champions League msimu wa 2013/14, Antoine Griezmann anaifukuzia rekodi hiyo akiwa ametupia kambani mara sita (6) hadi sasa.
  • Griezmann ameweza kufunga kwa mara nyingine tena kwenye michezo miwili dhidi ya timu moja, laifanya hivyo dhidi ya Galatasaray kabya ya Barcelona.
  • Barcelona wameshindwa kufunga goli kwenye mchezo wa Champions League kwa mara ya kwanza tangu April 2014 mchezo ambao pia ulikuwa ni dhidi ya Atletico Madrid.