DODOMA FM NA ABM RADIO VITUO PEKEE MKOANI DODOMA VILIVYO TEULIWA KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA TUZO ZA MCT/EJAT. - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Wednesday, 13 April 2016

DODOMA FM NA ABM RADIO VITUO PEKEE MKOANI DODOMA VILIVYO TEULIWA KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA TUZO ZA MCT/EJAT.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MCT yatangaza majina ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015


* Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tom Nyanduga kuwa Mgeni Rasmi
Kamati ya maandalizi ya EJAT 2015 leo limetangaza majina 84 ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015. Idadi hiyo ni ongezeko la wateule 31 ukilinganisha na tuzo za 2014 ambapo wateule walikuwa ni 53 tu.


Pia kamati imeeleza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tom Bahame Nyanduga ndio Mgeni Rasmi kwenye Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT ) 2015 zitakazofanyika kwenye tamasha la usiku la utoaji wa tuzo hizo Aprili 29, 2016 , Dar es Salaam.
Kutangazwa kwa wateule wa EJAT 2015 kunafuatia kukamilika kwa kazi ya kuzipitia na kuchagua zile zilizo na ubora zaidi iliyofanywa na jopo la majaji 10 lililokaa mwezi Machi mwaka huu. Majaji hao ambao ni wataalamu mbalimbali wa masuala ya habari walipitia kazi za kiandishi zaidi ya 570 zilizowasilishwa kwenye makundi ya kushindaniwa 22 kwenye tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015.
Ripoti ya jopo la majaji hao kuhusu wateule wa EJAT 2015, inaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa kwa wateule kwa upande wa luninga ambapo kuna wateule 27 kutoka wateule wawili katika tuzo za 2014. Pia kuna ongezeko kwenye wateule wa redio kutoka 17 hadi 27. Hata hivyo kwa upande wa magazeti wateule wamepungua kidogo kutoka wateule 34 wa tuzo za 2014 hadi 32 kwa tuzo za mwaka 2015.


Idadi ya wateule wanawake pia imeongezeka kufikia 28 kutoka wateule 18 kwenye tuzo za EJAT 2014. Pia ripoti inaonyesha kuongezeka kwa kazi zilizoletwa na redio za kijamii mwaka huu ambapo baadhi yao zimeweza kutoa wateule kwenye tuzo za EJAT 2015.


Jopo hilo la majaji liliongozwa na mwenyekiti wake, Bi. Valerie Msoka, wajumbe wengine walikuwa Dk. Joyce Bazira Ntobi ambaye alikuwa katibu wa jopo, na Ali Uki. Wanajopo wengine walikuwa Jesse Kwayu, Kiondo Mshana, Juma Dihule, Godfrey Nago, Nathan Mpangala na Pili Mtambalike. Waandishi hao 84 wataingia kwenye kinyang’anyiro cha mashindano ya EJAT 2015.
Majaji hao 10 waliapishwa na Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo Machi 11, 2016 kabla ya kuanza kazi hiyo. Hii itakuwa ni mara ya saba


kuwatuza waandishi waliofanya vizuri katika kazi zao za kiuandishi chini ya utaratibu wa EJAT.Sambamba na EJAT, Jopo la wataalam kwa ajili ya Tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika Uandishi wa Habari (LAJA) umeanza kazi ya kutafuta mteule wa tuzo hiyo kwa mwaka huu ambae atatangazwa wakati wa Tamasha hilo la usiku. Jopo la LAJA linalongozwa na Mwenyekiti wake Bi. Lilian Kallaghe lina wajumbe watano ambao ni pamoja na Hamis Mzee, Fili Karashani, Joseph Kulangwa na Wenceslaus Mushi.
Makundi yaliyoshindaniwa ni yafuatayo:
1. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchumi na Biashara
2. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Michezo na Utamaduni
3. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Mazingira
4. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Afya
5. Tuzo ya Uandishi wa Habari za VVU/Ukimwi
6. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Watoto
7. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utawala Bora
8. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Jinsia
9. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Sayansi na Teknolojia
10 Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi
11. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Afya ya Mama na Mtoto
12. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Elimu
13. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utalii na Uhifadhi
14. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Watu Wenye Ulemavu
15. Mpiga Picha Bora – Magazeti
16. Mpiga Picha Bora – Runinga
17. Mchora Katuni Bora
18. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kilimo
19. Tuzo ya Afya ya Uzazi kwa vijana
20. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini
21. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Manunuzi ya Umma
22. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kodi na Ukusanyaji Mapato
Ifuatayo ni orodha ya wateule wa EJAT 2015 ambao wanatoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari

WATEULE WA EJAT 2015
SN JINA LA MWANDISHI CHOMBO CHA HABARI MKOA ANAOTOKA
1. Sylvester Joseph Afya Radio Mwanza
2. Fatuma Mtengamani Ulanga FM Ulanga-Mahenge (Morogoro)
3. Adam Hhando CG FM Tabora
4. Abisae Maeda TV1/Kilimanjaro Film Institute Arusha
5. Mwashamba Juma Zanzibar Leo Zanzibar
6. Jackline Masinde Mwananchi DSM
7. Peter Rodgers ITV Mwanza
8. Lucas Maziku Star TV Mwanza
9. Maajabu Madiwa Pangani FM Pangani-Tanga
10. Ezekiel Kamanga BBC & Bomba FM Mbeya
11. Malongo Mbeho Metro FM Mwanza
12. Annastazia Maginga Raia Tanzania Mwanza
13. John Leon Lewanga TBC DSM
14. Mussa Kinkaya Sunrise FM Arusha
15. Victor Makwawa Dodoma FM Dodoma
16. Pili Mlindwa Pangani FM Pangani-Tanga
17. Zulfa Golay Mwananchi Arusha
18. Tumaini Msowoya Mwananchi Iringa
19. Nuzulack Dausen The Citizen DSM
20. Haji Mohamed Zanzibar Leo Pemba-Zanzibar
21. Silvano Kayera Mlimani DSM
22. Christian Msafiri CG FM Tabora
23. Grace Mbise Bomba FM Mbeya
24. Salome Kitomari Nipashe DSM
25. Kelvin Matandiko Mwananchi DSM
26. Mansour Jumanne SAUT FM Mwanza
27. Frank Bahati TBC1 DSM
28. Khamis Suleiman Channel Ten DSM
29. Emmanuel Buhohela ITV DSM
30. Lusekelo Philemon The Guardian DSM
31. John Nsuza TV1 Arusha
32. Esther Zelamula Channel ten DSM
33. Elibahati Akyoo TV1/ Kilimanjaro Film Institute Arusha
34. Idd Juma Afya Radio Mwanza
35. Mashaka Mgeta The Guardian DSM
36. Kisali Simba Star TV Shinyanga
37. Editha Kinyaiya TV1/Kilimanjaro Film Institute Arusha
38. Emmanuel Kitomari TV1/Kilimanjaro Film Institute Arusha
39. Maulid kambaya Radio One DSM
40. Lulu George Nipashe Tanga
41. Mussa Siwayombe Mwananchi Arusha
42. Victor Eliah TBC DSM
43. Cassius Mdami Channel Ten DSM
44. Anthony Masai Triple A FM Arusha
45. Temigunga Mahondo Radio Country FM Iringa
46. Beatrice Shayo Nipashe DSM
47. Rahma Suleiman Nipashe Zanzibar
48. Haika Kimaro The Citizen DSM
49. Halfan Lihundi ITV Arusha
50. Lydia Igarabuza EATV DSM
51. Valeria Mwalongo Tumaini DSM
52. Peninah Kajura HHC Radio Mwanza
53. Goodluck Mvamba SAUT FM Mwanza
54. Said Michael Mtanzania DSM
55. Abdul Kingo Nipashe DSM
56. Nora Damian Mtanzania DSM
57. Sauli Gilliard The Citizen DSM
58. Alfayo Misiyeki TV1/Kilimanjaro Film Institute Arusha
59. Samson Kapinga TV1/ Kilimanjaro Film Institute Arusha
60. Florence Majani Mwananchi DSM
61. Selemani Mkufya TBC1 DSM
62. Kasilda Mgeni Star TV Morogoro
63. Tuma Dandi Mlimani DSM
64. Eveline Mhozya CG FM Tabora
65. Vivian Pyuza CG FM Tabora
66. Joseph Mwendapole Nipashe DSM
67. Hadija Jumanne Mwananchi DSM
68. Christina Mwakangale Nipashe DSM
69. Sanula Athanas Nipashe DSM
70. Mwanahiba Richard Mwanaspoti DSM
71. Japhary Ramadhan ABM FM Dodoma
72. Bernard Lugongo The Citizen DSM
73. Emmanuel Mollel TV1/ Kilimanjaro Film Institute Arusha
74. Joel Ulomi Arusha One Arusha
75. Haji Nassor Zanzibar Leo Chake Chake-Pemba
76. Peti Siyame Habari Leo Sumbawanga-Rukwa
77. Robert Okanda Dailynews DSM
78. Nuru Hassan Afya Mwanza
79. Shija Felician The Citizen Kahama
80. Salum Maige Mwananchi Geita
81. Projestus Binamungu Star TV Mwanza
82. Regina Kulindwa Afya Mwanza
83. Denis Nyali Nuru Iringa
84. Sam Mahela ITV DSM


Waandaaji wa EJAT 2015 ni pamoja na Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika- Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri (TEF), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), Chama cha Waandishi wa Habari Walio katika Mapambano Dhidi ya UKIMWI Tanzania (AJAAT), Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), PSI-Tanzania, Unicef, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Haki Elimu, SIKIKA, Evidence for Action, Amref Health Africa na BESTDialogue/ANSAF.
Kajubi D. Mukajanga
Mwenyekiti
Kamati ya Maandalizi ya EJAT 2015