YOUNG DEE AIZUNGUMZIA KOLABO YAKE NA DIAMOND PLATNUMZ ILIVYO FELI - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Thursday, 17 March 2016

YOUNG DEE AIZUNGUMZIA KOLABO YAKE NA DIAMOND PLATNUMZ ILIVYO FELI

Katika kufanikisha mipango ya kufanya kolabo na Daimond Platnumz, Young Dee aliandaa nyimbo aliyoipa jina la UJANJA UJANJA ambayo  Diamond alikuwa tayari amesha andaa kiitikio lakini haikuwezekana kwa kuwa Diamond alibanwa na ratiba na wakati huo huo nyimbo ilitakiwa kutoka na hivyo kulazimika kuachia nyimbo hiyo.young-Dee

Hata hivyo rapa huyo ameweka wazi kuwa bado ana matarajio ya kufanya kazi na Diamond Platnumz licha ya mpango wake kushindikana kwa mwaka huu, jambo ambalo amewataka wasanii wenzake kumtumia Diamond Platnumz badala ya kukukimbilia wasanii wa nje ya Tanzania wakati hata wao baadhi yao wanataka kufanya kazi na Diamond Platunumz na kuongeza kuwa yeye anaitaka kolabo ya Diamond kuliko hata ya msanii wa kimarekani T-pain.

Ukiachilia mbali suala hilo Young Dee ameiambia www.mtembezi.comkuwa mwaka 2015 kwake umekuwa mwaka wa mafanikio makubwa na anatarajia mwaka 2016 uatakuwa ni mara mbili zaidi ya 2015, na hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa vitu vizuri anavyo waandalia